Thursday May 23, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Okwi atua Orlando Pirates

15th June 2012
Print
Comments
Emmanuel Okwi

Klabu ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini juzi imetuma rasmi barua kwa uongozi wa Simba ikimtaka mshambuliaji wake, Emmanuel Okwi, aende kufanya majaribio katika timu hiyo ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini.

Akizungumza na gazeti hili jana, Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu' alisema kuwa wamepokea barua hiyo na watamruhusu Okwi aende kufanya majaribio kwenye timu hiyo.

Kaburu alisema kuwa Okwi atajiandaa na safari hiyo muda mfupi baada ya kurejea nchini akitokea kwao Uganda aliko sasa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uganda (Cranes).

Alisema kuwa klabu ya Orlando Pirates itamfanyia majaribio kwa muda wa wiki mbili na tayari imeshatuma barua ya kumuombea viza ya kuingia Afrika Kusini kwa sababu Okwi ni raia wa Uganda na hivyo anahitaji kupata viza.
"Kwa sasa Simba tunafanya usajili wetu kimya kimya, ila pia tuko mbioni kumuuza Okwi mipango ikienda sawasawa," alisema Kaburu.

Kiwango cha Okwi aliyezaliwa Desemba 25 mwaka 1992, kimeonekana kupanda zaidi kuanzia mwaka jana na tayari amekuwa akianza kwenye kikosi cha kwanza cha Cranes katika mechi za timu hiyo za hivi karibuni tofauti na ilivyokuwa huko nyuma.

Kaburu alisema vilevile kuwa Simba itaingia kambini mwishoni mwa mwezi huu.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment