Thursday Jun 20, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Mbowe, Lema wajisalimisha polisi
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema wamejisalimisha leo katika kituo Kikuu cha Polisi Mkoani Arusha kwa ajili ya kuhojiwa.

Simba yakanusha kuacha wachezaji

2nd June 2012
Print
Comments
Makamu mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu'

Makamu mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu' amesema uongozi wa klabu hiyo haujaamua wachezaji watakaoachwa katika usajili wa msimu ujao wa ligi kuu ya Bara.

Kauli hiyo ya Kaburu imekuja kufuatia uvumi wa kuwepo kwa orodha ya majina ya wachezaji ambao wameachwa na klabu hiyo.

Kaburu alisema kuwa kamati ya ufundi pamoja na kamati ya usajili ya klabu hiyo zipo kwenye upembuzi wa ripoti ya kocha Milovan Cirkovic kujua wachezaji gani wa kuongezwa na wachezaji gani wa kuachwa kwenye kikosi hicho.

"Kama ni usajili tutafanya hivyo kwa kufuata ushauri na maelekezo ya kocha wetu" alisema Kaburu.
"Mpaka sasa hatujatangaza wachezaji wa kuachwa... hilo bado lipo ndani ya uongozi."

Alisema kutokana na ripoti ya kocha Milovan, wapo wachezaji kwenye kikosi hicho ambao kuna uwezekano wa kuachwa kutokana na uwezo wao kushuka.

Pia alisema baadhi ya wachezaji wa klabu hiyo mikataba yao inamalizika mwezi ujao ambapo wapo watakaoongezewa na wengine wataachwa kutokana na maelekezo ya kocha.

"Kwa sasa hivi Simba haijaacha mchezaji yoyote, viongozi wanafanya kazi yao na muda ukifika kila kitu kitakuwa wazi ila tu niweke wazi kuwa wapo wachezaji tutakaowaacha na wapo tutakaowasajili," aliongezea kusema Kaburu.

Katika hatua nyingine, Katibu wa Simba, Evodius Mtawala walisema kuwa klabu hiyo tayari imeanza maandalizi ya awali kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu ambapo wachezaji wa klabu hiyo waliokuwa kwenye mapumziko wameanza kuwasili jijini kuanza maandalizi hayo.
 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment