Saturday Apr 30, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Mwasikili hatihati Twiga

23rd May 2012
Print
Comments
Timu ya soka ya taifa ya wanawake ya Tanzania Twiga Stars

Timu ya soka ya taifa ya wanawake ya Tanzania (Twiga Stars) inaondoka nchini kesho kwenda jijini Addis Ababa kwa ajili ya mechi yake ya kwanza ya kusaka tiketi ya kushiriki fainali zijazo za Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya wenyeji wao Ethiopia itakayofanyika Jumapili nchini humo.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Boniface Wambura, alisema kuwa timu hiyo itaondoka na ndege ya Shirika na Ndege la Ethiopia ambapo wachezaji watakuwa ni 20 pamoja na viongozi watano wa benchi la ufundi.

Wambura alisema kuwa bado shirikisho liko katika mawasiliano na Chama cha Soka cha Uturuki ili kuweza kumpata beki wake, Sophia Mwasikili, ili kujua ataungana na wenzake lini kwa ajili ya mechi hiyo muhimu. "Bado hatujajua ni lini atakuja mpaka sasa tunasubiri mawasiliano nao, ila yuko katika mpango wa kocha Mkwasa (Boniface)," alisema Wambura.

Katika kujiandaa na mechi hiyo Twiga Stars imecheza mechi mbili za kirafiki za kimataifa ambapo ya kwanza ililala magoli 4-1 dhidi ya Zimbabwe na Jumapili iliyopita ikapokea kichapo cha 5-2 kutoka kwa Afrika Kusini (Banyana Banyana).
SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles