Friday May 6, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

SMZ kufanya mabadiliko makubwa serikali za mitaa

7th May 2012
Print
Comments
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein

Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, amesema serikali yake inatarajia kufanya mabadiliko makubwa ya serikali za mitaa na mikoa, ili kuimarisha utoaji wa huduma na kuondoa uzembe na uvivu katika maeneo ya kazi.

Aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini `B', baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la ghorofa ambalo litatumika kama makao makuu ya halmshauri hiyo, mradi ambao unatarajiwa kugharimu Sh. milioni 300 hadi kukamilika kwake, huko Kitope, mkoa wa Kaskazini Unguja.

Dk. Shein alisema mabadiliko ya serikali za mitaa na mikoa, tayari yamefanyika kwa upande wa Tanzania Bara, na yameanza kuleta mafanikio makubwa katika utekelezaji wa shughuli za serikali, na utoaji huduma kwa wananchi.

Dk. Shein alisema chini ya mabadiliko hayo watumishi wa umma watapewa kazi kwa mikataba badala ya kuwa waajiriwa wa kudumu, lengo likiwa ni kuwawezesha kujipima wenyewe katika utendaji wa kazi.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles