Tuesday May 3, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Ashanti, Polisi Mara kufungua dimba

26th May 2012
Print
Comments
Afisa Habari wa Shirikisho la soka nchini (TFF)Boniface Wambura,

Timu  za soka za Ashanti United na Polisi Mara zimepangwa kufungua pazia la michuano ya ligi ya Taifa inayoshirikisha timu bingwa za mikoa ya Bara.

Michuano ya Ligi ya Taifa imepangwa kuanza kesho katika vituo vitatu tofauti huku timu hizo za Ashanti na Polisi Mara zikifungua pazi kwenye kituo cha Musoma.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la soka nchini (TFF) iliyotolewa na Afisa Habari wake, Boniface Wambura, ligi hiyo ambayo inatarajia kumalizika Juni 13 mwaka huu itashuhudia mechi mbili kwa siku katika kila kituo, huku ya kwanza ikichezwa saa 8 mchana na kufuatiwa na mchezo wa pili utakaokuwa ukianza saa 10 jioni.

"Kwa mechi za ufunguzi katika kituo cha Musoma, mechi mbili zitachezwa ambapo Asahanti ya Dar es Salaam itapambana na Polisi Mara ambapo mchezo huo utatanguliwa na mchezo kati ya Flamingo ya Arusha dhidi ya Forest ya Kilimanjaro na michezo yote itachezwa kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma," ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Katika kituo cha Kigoma, kesho kutakuwa na mchezo mmoja utakaoanza saa 10 jioni kwenye uwanja wa Lake Tanganyika, ambapo timu ya Mwadui ya Shinyanga itapambana na JKT Kanembwa ya Kigoma.
Siku inayofuata kwenye kituo hicho timu ya CDA ya Dodoma itapambana na Majimaji ya Tabora wakati Bandari ya Kagera itaumana na Pamba ya Mwanza.

Kwenye kituo cha Mtwara, timu ya Tenende ya Mbeya itapamaba na Kurugenzi ya Iringa kesho kwenye mchezo wa kwanza ambapo mchezo wa pili timu ya Mpanda Stars ya Rukwa itapambana na Ndani ya Mjini Mtwara kwenye uwanja wa Umoja mjini Mtwara.
 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles