Monday May 2, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Pinda aukwepa mgogoro wa kahawa

14th May 2012
Print
Comments
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amewaweka njia panda viongozi wa serikali ya mkoa wa Mbeya, baada ya kuwaagiza mgogoro u wa muda mrefu kuhusu ununuzi wa kahawa mbivu upelekwe kwa wananchi ambao ndio watakaoamua utaratibu upi utumike wakati wa kuuza kahawa kwa makampuni yanayonunua zao hilo.

Ametoa agizo hilo baada ya kuelezwa na Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, kuhusu msimamo uliowekwa na serikali ya mkoa kwamba ni marufuku kwa makampuni binafsi kununua kahawa mbivu (mbichi) kwa wakulima kwasababu hali hiyo inawanyonya wakulima.

Kufuatia msimamo huo wa serikali ya mkoa kumekuwa na mvutano mkali uliodumu kwa muda mrefu kati ya Halmashauri za Wilaya, Serikali ya mkoa, Wizara ya Kilimo na Chakula na baadhi ya makampuni yanayonunua kahawa hasa kutokana na zuio hilo kudaiwa kulenga baadhi ya makampuni tu.

Hata hivyo, Pinda alisema mgogoro huo wa ununuzi wa kahawa umechukua muda mrefu bila kupatiwa ufumbuzi kutokana na baadhi ya viongozi kujihusisha na kukuza mgogoro sababu wao nao wanafanya biashara ya kahawa mbivu.

Uamuzi huo wa Waziri Mkuu umepokelewa kwa furaha kubwa na wakulima ambao wamedai alichokisemani sahihi kwani baadhi ya viongozi kupitia  ndugu zao wana makampuni yanayonunua kahawa mbivu lakini wameng’ang’ania kuzuia baadhi ya makampuni.

Hivi karibuni Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ilidaiwa kuandika barua ya kuondoa zuzio lililokuwa limewekwa na uongozi wa serikali ya mkoa wa Mbeya wa kupiga marufuku ununuzi wa kahawa mbichi.

Kwa mujibu wa barua hiyo yenye kumbu Na.HA.79/334/02/07/14 ya Aprili 10 mwaka huu iliyosainiwa na D.I Bandisa kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Tamisemi iliondoa zuio hilo, lakini hata hivyo serikali ya mkoa wa Mbeya ilikataa barua hiyo kwa kueleza kuwa ni ya kufoji na kuagiza waliohusika kuisambaza wachukuliwe hatua ingawa hadi sasa hakuna aliyekamatwa.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles