Friday May 6, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Katibu wa CCM auawa Mwanza

12th May 2012
Print
Comments

Katibu wa CCM Tawi la Isunga katika Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza, Marco Manyilizu (47) ameuawa kwa kupigwa na fimbo kichwani.

Kiongozi huyo alishambuliwa wakati akikusanya michango kwa ajili ya kufanikisha uchaguzi wa viongozi wa tawi hilo.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Deusdedith Nsimeki,  aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa mauaji hayo yalitokea juzi Alhamis  saa 1:00 usiku katika kijiji cha Isunga na kumtaja muuaji kuwa ni Marco Gervas (31).

Alifafanua kwamba siku ya tukio, Manyilizu maarufu kwa jina la Kiroma alikuwa ameongozana na katibu wake wa Masuala ya Uchumi, Esther Elias (42) ambaye ni mke wa mtuhumiwa Gervas.

Alidai kuwa alipigwa na mtuhumiwa huyo wakati anarejea nyumbani  kutoka   kukusanya michango hiyo.
Gervas alimvamia Manyilizu na kuanza kumshambulia kwa fimbo kichwani, ambapo marehemu alikimbia  kuelekea kwake lakini alidondoka njiani na kufariki papo hapo.

Kwa mujibu wa Kamanda Nsimeki, baada ya tukio hilo wananchi walimkamata Gervas na kumpelekea katika kituo kidogo cha Polisi cha Sumve.

Hata hivyo,  alidai kuwa wakiwa njiani kuekelea kituoni  alitoroka katika mazingira ya kutatanisha hali inayoonyesha kuwa baadhi ya wananchi walifanya mpango wa kumtorosha kwa makusudi.

Kufuatia tukio hilo, Nsimeki alisema Polisi imewatia mbaroni Nyanda Elias (36) ambaye ni Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mapembe, Robert Shineneko (32) ambaye ni rafiki wa mtuhumiwa pamoja na askari wa sungusungu   kijijini hapo Sihaile Buswelu (30).

Alisema  watu hao watatu wanatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya upelelezi wa awali kukamilika kwa tuhuma za kumsaidia mtuhumiwa wa mauaji kutoroka.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles