Wednesday May 22, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Misri waikacha Ngorongoro kirafiki

3rd July 2012
Print
Comments
Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura

Timu ya soka ya vijana ya umri chini ya miaka 20 ya Misri imekacha kuja nchini kuivaa Ngorongoro Heroes katika mechi mbili za kirafiki zilizopangwa kufanyika leo na keshokutwa Alhamisi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Chama cha Soka cha Misri (EFA) jana kilituma taarifa za kutokuja kwa yosso hao na kueleza kwamba watakuwa tayari kuja tena nchini katikati ya mwezi ujao.

Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, alisema jana kuwa mechi nyingine za kirafiki kati ya Ngorongoro Heroes dhidi ya wenzao wa Rwanda zinazotarajiwa kufanyika Julai 14 na 16 mwaka huu nchini zipo kama kawaida.

Wambura alisema Ngorongoro Heroes imetafutiwa mechi hizo kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wake wa raundi ya pili dhidi ya Nigeria utakaofanyika Julai 28 nchini na marudiano baada ya wiki mbili jijini Lagos ambapo wanasaka tiketi ya kucheza fainali za Afrika kwa vijana.

Alisema Ngorongoro Heroes ambayo sasa iko chini ya kocha mpya, Michelsen Jakob, itaendelea na mazoezi yake na maamuzi ya kuwavaa yosso wa Misri yatategemea programu za kocha huyo itakavyoeleza wakati huo.

Wakati huo huo, Kamati ya Uchaguzi ya TFF imekubali maombi ya kupelekea mbele uchaguzi wa Chama cha Soka cha mkoa wa Dar es Salaam (DRFA).

Sasa mchakato wa uchaguzi wa DRFA utaanza rasmi Julai 15 wakati wenzao wa Kigoma (KRFA) wameomba wafanye uchaguzi wao Septemba Mosi mwaka huu.

Vyama mbalimbali vya soka na wanachama wengine wa TFF wanafanya chaguzi zao ili waweze kupata viongozi watakaoshiriki kwenye mkutano mkuu wa shirikisho hilo utakaofanyika mwezi Desemba mwaka huu.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment