Sunday May 1, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Makala atoa mamilioni ujenzi wa masoko ya kisasa

22nd May 2012
Print
Comments
Naibu Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Amos Makalla

Naibu Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Amos Makalla,ametoa shilingi milioni 20 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa masoko katika kata ya Mvomero, Dakawa, Mlali na Kibati wilayani Mvomero Mkoani Morogoro.

Makalla ambaye ni Mbunge wa Jimbo hilo amekabidhi hundi za Sh. milioni 5 kwa kila kata ili kuwezesha kuanza kwa mchakato wa ujenzi wa masoko ya kisasa katika maeneo yaliyotengwa  wakati wa ziara yake ya kukagua na kuhimiza maendeleo kwa wananchi wa wilaya hiyo.

Mbunge huyo alitaka  mpango wa ujenzi wa masoko hayo  uanze kufanyika mara moja ikiwa na kuweka  makadiriko ya gharama za ujenzi.

Kata ya Mvomero ilikuwa ya kwanza  kukabidhiwa wakati wa   mkutano  wa hadhara uliofanyika hivi karibuni   na pia kuuagiza uongozi wake kuanza mchakato wa ujenzi wa soko la kisasa litakaotumiwa na wananchi wa ndani na nje ya kata ili kwenda na kasi ya ukuaji wa mji huo.

Aliwataka wananchi kwa kushirikianana uongozi wao na nguvu za Mbunge atakapofikisha hatua nzuri ya ujenzi itakuwa ni  rahisi kuwashawishi wadau wengine kuchangia ujenzi huo  pamoja na  Halmashauri ya Wilaya kutenga  bajeti ya fedha za kuendeleza ujenzi huo.

“ Huu ni mkakati wangu  na ni miongoni mwa kero zilizotolewa na wananchi juu ya ukosefu wa masoko “ alisema Mbunge huyo .

Mbunge huyo alitoa hundi za kiwango kama hicho kwa viongozi wa Serikali ya  Kata ya Kibati, Dakawa na Mlali na kusema masoko hayo yakikamilishwa yatawanufaisha wakulima na wananchi katika mifumo mizuri ya   bei  ya mazao .

Hata hivyo aliwaonya Viongozi wa Serikali za Vijiji  na Kata hizo ,kuwa fedha hizo zisitumiwe katika shughuli nyingine kinyume na ilivyokusudiwa na viongozi watakaokiuka utaratibu watawajibishwa.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles