Friday May 6, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Marwa ashindwa kufuzu Olimpiki

3rd May 2012
Print
Comments
Mwanariadha Dickson Marwa

Mwanariadha Dickson Marwa ameshindwa kufuzu kushiriki michezo ya Olimpiki baada ya kushidwa kufanya vizuri katika mashindano ya marathon ya Hamburg yaliyofanyika Machi 29 nchini Ujerumani.

Marwa ambaye amerejea jijini Dar es Salaam jana, aliondoka April 26 kuelekea nchini humo.

Akizungumza na NIPASHE jana, katibu wa chama cha riadha nchini (RT), Suleiman Nyambui alisema mwanariadha huyo ameshindwa kumaliza kilomita 42 baada ya kukimbia km. 38 na kushindwa kuendelea.

Nyambui alisema sababu za mwanariadha huyo kushindwa kumaliza mbio hizo, ni kutokana na kusumbuliwa na malaria.

"Marwa ameingia jijini jana, anadai ameshindwa kumaliza mbio hizo kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa malaria," alisema Nyambui.

Nyambui alisema kwa mujibu wa Marwa, alidai aliondoka nchini huku akisumbuliwa na malaria lakini alitaka kujaribu bahati yake.

Kushindwa huko kunamaanisha kwamba Tanzania ina wanariadha wawili waliofuzu kushiriki katika michezo ya Olimpiki ambao ni Samson Ramadhan (marathon) na Zakia Mrisho anayekimbia mita 5,000.

Nyambui alisema bado wanafuatilia matokeo ya mwanariadha Faustine Musa ambaye alifuzu kushiriki michezo ya Olimpiki, lakini bado matokeo yake hayajarejeshwa na shirikisho la riadha duniani (IAAF).

Nyambui alisema endapo matokeo yake yatarejeshwa mapema, Faustine ataungana na wanariadha waliofuzu kushiriki michezo ya Olimpiki, kuendelea na mazoezi ya kujiandaa na mashindano hayo.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles