Monday May 2, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Ugonjwa wa kuhara hadi kufa wazuka

5th May 2012
Print
Comments

Ugonjwa mpya wa kuhara hadi kufa unaowashambulia watoto umeingia nchini katika wilaya ya Muheza mkoani Tanga.
Ungojwa huo mpya unasababishwa na virusi vinavyojulikana kama LUTA VIRUS.

Mwakilishi wa Shirika la Afya duniani (WHO) anayeshughulikia masuala ya chanjo Dk. Christopher Kamugisha, alisema kuwa ugonjwa huo umegundulika nchini mwa mwanzoni mwa mwaka huu wilayani Muheza baada ya watoto wachanga waliokuwa wanaharisha kupimwa na kubainika kuwa nao.

Alisema hadi kufika jana, ugonjwa huo huenda ukawa umeshasambaa hadi katika jiji la Dar es Salaam baada ya kupata taarifa kuwa kuna watoto wamelazwa katika hospitali mbili za jiji hilo wanaugua ugonjwa wenye dalili kama za ugonjwa huo.

Alisema WHO kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wanatarajia kuanza kutoa chanjo hiyo hapa nchini Januari mwakani.
 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles