Wednesday May 4, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Vifaa vya Dart vyaruhusiwa bandarini

18th May 2012
Print
Comments

Vifaa kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa mabasi yaendayo kasi jijini Dar es Salaam (DART), vilivyokuwa vimekwama bandarini , vimeanza kutoka baada ya mazungumzo kati ya Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Msemaji wa Wizara ya Ujenzi, Martin Ntemo, aliliambia NIPASHE kuwa vifaa hivyo vilianza kutoka tangu wiki iliyopita ili mradi huo uweze kutekelezwa baada ya kukutana na changamoto mbalimbali.

Jitihada hizo zimefanyika baada ya Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, kutembelea ujenzi wa mradi huo na kuelezwa na Mkandarasi aliyepewa zabuni ya kujenga barabara hizo Kampuni ya Stra Bag ya nchini Ujerumani kumweleza kuwa baadhi ya changamoto wanazozipata ni vifaa kukwama bandarini.

“Vifaa vilivyokuwa vimekwama bandarini kama Waziri alivyoelezwa tayari vilishaanza kutoka tangu wiki iliyopita kwa hilo hatuna tatizo nalo tunaendelea kushughulikia changamoto nyingine kuhakikisha mradi haukwami,” alisema Ntemo.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles