Sunday May 26, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Bidhaa Duni

26th June 2012
Print
Comments

Serikali  ya China imewaasa wafanyabiashara wa Kitanzania wanaoenda kununua bidhaa nchini humo kuachana na tabia ya kununua bidhaa zenye ubora wa chini, zinazouzwa kwa bei ‘chee’ kwa ajili ya kuziingiza kwenye soko la Tanzania kwa tamaa ya kupata faida kubwa huku wakiwapa walaji bidhaa zisizo na viwango.

Wito huo ulitolewa jana jijini Dar es salaam na Lin Zhiyong, Mwakilishi wa Masuala ya Uchumi na Biashara wa nchi hiyo nchini, wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na maonyesha makubwa ya kibiashara yaliyoandaliwa na nchi hiyo kwa mara ya kwanza barani Afrika.

Maonyesho hayo yanayoanza Julai Mosi hadi 5, Mwaka huu yatafanyika katika viwanja mwa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam, yakihusisha bidhaa mbalimbali zikiwemo mashine, magari, vifaa vya umeme, vifaa vya nyumbani, vyombo vya mawasiliano, elektroniki, nishati ya jua, bidhaa za matumizi ya kila siku, vifaa vya ujenzi, kemikali na huduma za afya za kisasa.


 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment