Saturday May 7, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Sekta binafsi, Marekani kuendeleza kilimo

24th May 2012
Print
Comments

Sekta binafsi nchini kwa kushirikiana na watu wa Marekani kupitia Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Marekani (USAID) wamekubalina kuendeleza ukuaji wa kilimo nchini kwa kuwasaidia wakulima ili kuongeza kiwango cha uzalishaji.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la kukuza kilimo katika Mikoa ya Kusini (SAGCOT), Danstan Mrutu, alisema ushirikiano kati ya wakulima na sekta binafsi ni njia pekee itakayosaidia kukuza na kuendeleza kilimo.

“Ushirikiano huu utasaidia kuhama kutoka kwenye kilimo cha biashara kwenda kilimo cha ushirikiano ambacho kinalenga kumsaidia mkulima mdogo,” alisema Mrutu.

Alisema wakulima wakishirikiana vyema na sekta binafsi wataweza kupata pembejeo za kilimo kutoka ambazo zitawasaidia katika kuzalisha zaidi na hivyo kuongeza kipato.

“Wakulima watatakiwa kujigawa katika makundi tofautitofauti ya wakulima wa mahindi, mchele, miwa, mihogo na wafugaji ili kupata misaada ya kifedha, soko na pembejeo za kilimo kutoka kwa mashirika ya kimataifa kupitia sekta binafsi,” alisema Mrutu.

Kwa upande, wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Biashara ya Mbegu za Mazao (Tanseed), Isaka Mashauri, alisema matumizi ya mbegu zilizo bora yatasaidia kuzalisha chakula bora cha kutosha, ambapo itasaidia kupunguza gharama za maisha ambazo zimekuwa zikiongezeka kila siku.

“Tuna uhakika na mpango huu mzuri wenye lengo la kuondoa umaskini na kuongeza kipato kwa wakulima, hata hivyo uzalishaji ukiongezeka tutaweza kuuza chakula kwa nchi nyingine za jirani,” alisema.

 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles