Monday May 2, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Simba kutembezwa wazi jijini

26th May 2012
Print
Comments
Kikosi cha Simba

Naibu  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makala, kesho anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za ubingwa za klabu ya Simba zitakazofanyika Mbagala jijini ambako wachezaji watawasili wakiwa katika gari la wazi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Geofrey Nyange 'Kaburu' alisema kuwa mbali na Makala viongozi mbalimbali ambao ni mashabiki wa klabu hiyo watakuwepo katika sherehe hizo ambazo zitaenda sambamba na kumuenzi aliyekuwa mchezaji wa timu hiyo Patrick Mafisango.

Aliwataja viongozi wengie ambao watakuwepo kwenye sherehe hizo za ubingwa kuwa ni pamoja na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki, Samuel Sitta pamoja na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.

"Hao ni baadhi tu ya viongozi wetu ambao ni mashabiki wa Simba watakaokuwepo pamoja na wachezaji kwenye sherehe za ubingwa wa timu yetu," alisema Kaburu.

Aidha, alisema kwenye sherehe hizo za ubingwa wachezaji wa timu hiyo watapita kwenye gari la wazi katika barabara mbalimbali za jiji la Dar es Salaam wakielekea Mbagala ambako kutafanyika sherehe hizo.

"Msafara utaanzia hapa klabuni na utaenda mpaka Magomeni kupitia barabara ya Morogoro ambako utasimama kwa muda kwenye tawi la Mpira Pesa na baadae utaelekea Ubungo kwenye tawi la Ubungo Terminal na na kurudi mpaka Magomeni na kuchukua barabara ya Kawawa kuelekea Karume na baadae Mbagala," alisema Kaburu.

Alisema mbali na kusherehekea ubingwa pia watatumia nafasi hiyo kuwatambulisha wachezaji wapya wa timu hiyo waliosajiliwa baada ya kumalizika kwa ligi kuu ya Bara.


 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles