Saturday Feb 6, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Kigogo wa CCM Arusha amfuata Millya Chadema

23rd April 2012
Print
Comments

Jinamizi la viongozi na Chama cha Mapinduzi (CCM) la kukihama chama hicho limeendelea kushika kasi, baada ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa wa Arusha, Justine Genda, naye kutangaza kukihamia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Genda ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa Kata ya Karatu Mjini, alitangaza uamuzi huo jana wilayani Karatu na tayari ameshapokelewa na viongozi wa Chadema katika hafla iliyohudhuriwa na Mwenyekiti wa Halimashauri ya Wilaya ya Karatu Titus Lazaro na Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Karatu, Thomas Darabe.

Genda alisema ameamua kujiunga na wanaharakati wa kupigania haki na kuleta mabadiliko na kuongeza kuwa kwa sasa fursa hiyo inapatikana  Chadema.

“Nimeamua kuhama CCM na kujiunga na Chadema na nina matumaini makubwa kwani  nimeona kuwa Chadema kuna fursa ya kumuwezesha kila mmoja kutoa mchango wake katika mchakato mzima wa mabadiliko na ni chama kinachoweza kuleta ukombozi wa kweli katika taifa,” alisema Genda.

Akizungumza baada ya kumkabidhi kadi ya Chadema mwanachama huyo, Lazaro aliwataka wanachama na viongozi zaidi wa CCM na vyama vingine wanaotaka mabadiliko ya kweli  kujiunga na Chadema kwani ni chama makini.

Katibu wa Chama Cha Tanzania Labour (TLP) Jimbo la Songea mkoani Ruvuma, Joseph Mkondora, amejiengua katika chama hicho na kujiunga na Chadema ambacho alisema ni chama pekee cha upinzani kinachoonyesha dira ya maendeleo kwa Watanzania.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment