Wednesday May 4, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Taarifa ya CAG yawaliza watumishi Magu

14th May 2012
Print
Comments
Mwenyekiti Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Augustino Lyatonga Mrema

Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi  Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) , imewaacha katika vilio na simanzi baadhi ya watumishi wa wilaya ya Magu baada ya kuadhibiwa kwa kukatwa tozo ya asilimia 15 kama adhabu kutokana na uzembe ulionyeshwa kwenye taarifa zao za fedha.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu, Cornel Ngudu-ngi, alisema kuwa taarifa iliyotolewa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Augustino Lyatonga Mrema Machi 29, mwaka huu, ilibaini kuwepo kwa makosa mbalimbali ya kitabu cha mahesabu cha halmashauri yakiwemo ya kiuchapaji, yale ya  kujumlisha tarakimu na makosa ya kujumlisha tarakimu.

Ngudu-ngi licha ya kukanusha kuwa halmashauri yake haijahusika na ubadhirifu wa kiasi cha Sh. bilioni 17 kama ambavyo iliripotiwa katika baadhi ya vyombo vya habari, lakini alikiri kuwepo kwa mapungufu makubwa kwenye taarifa yao ya fedha hatua iliyoifanya ofisi ya CAG kutoa adhabu ya tozo ya asilimia 15 kwa baadhi ya watumishi wa halmashauri hiyo.

“Baada ya kubainika kwa makosa hayo kwa mujibu wa taarifa ya CAG, tuliagizwa na LAAC tuandae upya mchanganuo wa mahesabu yetu kwa usahihi  ambapo tulifanya hivyo na tuliwasilisha mahesabu yetu kwa  CAG tangu Aprili 28, mwaka huu, lakini mimi na wakuu wangu wa idara tuliandikiwa barua za onyo zilizoelekeza tukatwe tozo ya asilimia 15 ya mishahara yetu ya mwezi wa nne ambayo tayari imeishakatwa,” alikiambia kikao cha baraza la madiwani na kuongeza:  “Kitabu chetu cha mahesabu cha Magu hakikujadiliwa na kamati, hivyo siyo kweli na siyo sahihi kusema kuwa kitabu kilionyesha upotevu wa Shilingi bilioni 17.”

Kwa mujibu wa ripoti ya LAAC iliyotolewa na Mkurugenzi wa wilaya Ngundu-ngi, ambayo Nipashe inayo nakala yake, imeyataja baadhi ya makosa hayo kuwa ni pamoja na kushindwa kuandikwa vyema kwa tarakimu za fedha Sh 81,376,625.97 ambayo iliweza kuandikwa Sh. 81,276,626.17, ukoseaji wa majina na vyeo, likiwemo jina la Mkurugenzi Mtendaji wa Hamashauri hiyo ambalo lilisomeka Ndugu-ngi badala ya Ngudu-ngi na kuwepo na maelezo ya aina tofauti tofauti yaliyohusika katika kufanya manunuzi kadhaa ya halmashauri.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles