Saturday May 25, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Dhuluma rambirambi za Mafisango Simba?

29th July 2012
Print
Comments
Marehemu Patrick Mafisango

Katika hali inayoonyesha fedha za rambirambi za marehemu kiungo Patrick Mafisango huenda zisitolewe na Simba kwa walengwa, klabu yake hiyo jana ilitoa sababu nyingine tofauti ya kuchelewa.

Katika mila za Kiafrika, michango ya rambirambi hutakiwa kukabidhiwa msibani ama si zaidi ya siku ya Arobaini tangu kufariki kwa marehemu.

Lakini ikiwa ni zaidi ya miezi miwili sasa, uongozi wa Simba jana ulitoa sababu ya tatu, tofauti, ya kutokabidhi fedha hizo ambazo baadhi ni michango ya kabla na siku ya kuaga mwili wa Mkongo huyo aliyefariki kwa ajali ya gari Mei 16, jijini.

Akizungumza na NIPASHE jumapili jana, Katibu Mkuu wa klabu hiyo Evodius Mtawala alisema Simba imepokea "barua yenye maelekezo" kutoka Wizara ya Mambo ya Nje juu ya malipo ya rambirambi hizo.

Lakini akaongeza haraka kwamba wiki hii watatoa taarifa rasmi juu ya barua hiyo ya Wizara.

Ni ajabu rambirambi za mtu binafsi kuingiliwa na Wizara ya Mambo ya Nje lakini Mtawala alisema, "unajua hili suala kidogo limekuwa kubwa.

"Taratibu zilikuwa tayari lakini tumepokea barua kutoka Wizarani na pia kuna maelekezo kutoka kwa ubalozi wetu kule Kongo.

"Sasa sisi kama Simba tumepanga wiki ijayo tutoe taarifa rasmi baada ya kuwasiliana tena na Wizara."

Msemaji wa Simba Ezekiel Kamwaga aliwahi kuiambia NIPASHE jumapili Juni kwamba klabu hiyo imekatazwa kutoa rambirambi hizo na Ubalozi wa Tanzania nchini JK Kongo.

Kiongozi huyo alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari siku chache baadaye akisema kwamba familia ya marehemu iliyopo Kinshasa imewatambulisha mtu wa kukabidhiwa fedha za rambirambi na ingefanya hivyo mapema iwezekanavyo.

Akitoka nje ya madai ya kwanza ya jana kwamba mapema wiki ijayo suala hilo lingepatiwa ufafanuzi baada ya kukutana na Wizara, Mtawala jana alisema pia:

Klabu hiyo itatoa ufafanuzi wa kukwama kwa rambirambi za Mafisango katika wiki maalum ya Simba hivi karibuni.

SOURCE: NIPASHE JUMAPILI
0 Comments | Be the first to comment