Friday May 24, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Wajipanga kupata faida, kujipanua

18th February 2013
Print
Mkurugenzi Mkuu wa ACB, John Lwande

Benki ya Biashara ya Akiba (ACB) imeweka malengo ya kupata faida kubwa katika mwaka huu.

 
Benki hiyo ambayo ilianzishwa na wajasiriamali wazalendo mwaka 1977, imejiwekea lengo la kupata faida ya Sh. bilioni tatu mwaka huu badala ya Sh. bilioni 1.6 iliyopatikana mwaka jana.
 
Akizungumza na wafanyakazi wa benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi Mkuu wa ACB, John Lwande, alisema benki hiyo inakusudia pia kupanua huduma zake kwa kuongeza matawi zaidi.
 
“Wiki chache zijazo yaani mapema mwezi Machi, tutafungua tawi letu Dodoma na baadaye tutafungua lingine mkoani Mwanza,” alisema.
 
Hata hivyo, alisema tayari benki hiyo ina matawi 15 ambayo ni ya Arusha, Moshi na mengine 13 ya Kijitonyama, Ubungo, Kariakoo, Buguruni, Tegeta, Kinondoni, Mbagala, Agrey, Tandale, Temeke, Ilala, Ukonga na tawi kuu jijini Dar es Salaam.
 
Lwande aliwapongeza wafanyakazi kwa kuisaida benki hiyo kupata faida kubwa mwaka jana na kuwataka wafanyekazi kwa bidii zaidi ili waweze kutimiza lengo la mwaka huu.
Katika hafla hiyo, wafanyakazi bora 10 wa benki hiyo walipewa vyeti pamoja na fedha taslimu.
 
ACB ilianza shughuli zake Agosti mwaka 1997 baada ya juhudi za wajasiriamali wazalengo 
 
 
 
SOURCE: NIPASHE