Saturday Apr 30, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Serikali yaanza kulipa deni la PPF

24th May 2012
Print
Comments

Mfumo wa hifadhi wa Mashirika ya Umma (PPF) umeanza kulipwa fedha iliyowekeza kwenye miradi mbalimbali ya serikali ikiwemo ujenzi wa jengo la Bunge, ofisa mwandamizi wa mfuko huo amesema.

Akizungumza katika majadiliano na wahariri Dar es Salaam jana, Meneja Mahusiano wa PPF, Lulu Mengele, alithibitisha kwamba fedha hizo zimeanza kulipwa kwa mujibu wa makubaliano na Serikali.

PPF imewekeza pia katika ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma, mradi unaoendelea ambao malipo yake hayajaanza kufanyika.

Ofisa huyo alisema mfuko unaruhusiwa kuwekeza kati ya asilimia tano na 30 ya mapato yake ya uwekezaji katika ujenzi wa majengo kwa ajili ya makazi, burudani na biashara.

Mbali ya uwekezaji huo, Lulu alisema mfuko umewezesha watoto zaidi ya 1,200 wa wanachama wake ambao wamefariki kupata elimu ambapo umeshatumia zaidi ya Sh. milioni 475 kukamilisha lengo hilo.

Kwa mujibu wa ofisa huyo, wanaonufaika na huduma hiyo ni watoto wanne wa mwanachama aliyefariki akiwa bado anafanyakazi na kwamba wanalipiwa ada kuanzia elimu ya awali hadi kidato cha nne.

Lulu alifafanua kwamba ada hulipwa moja kwa moja kwenye akaunti ya benki ya shule ya mtoto husika kila mwanzo wa mwaka wa kitaaluma.

 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles