Sunday May 1, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Chadema yamng`ang`ania Ngeleja

21st May 2012
Print
Comments
Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimepanga kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja na mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Mathew Lubongeja kwa madai kuwa wameshindwa kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Tamko hilo la Chadema limekuja siku chache baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kutoa agizo la kuhakikisha Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya ya Sengerema na Misungwi mkoani Mwanza wanachukuliwa hatua za kisheria kwa kuwafikisha mahakamani kwa kosa na ulaji wa fedha za umma.

Mbunge wa Nyamagana (Chadema), Ezekiel Wenje, akizungumza na wananchi wa kijiji cha katunguru, alisema lazima chama chake kiwaburuza mahakamani Ngeleja na Lubongeja .

Wenje alisema Mwenyekiti wa Halmashauri ya Sengerema kati ya mikataba 73 aliyoisaini 13 ni hewa suala ambalo alisema sio la kulifumbia macho.

Alisema Chadema hakiwezi kukaa kimya kwa kulifumbia macho suala hilo na kwamba serikali inapaswa kuwafikisha makamani haraka kabla ya chama hicho hakijachukua uamuzi mgumu wa kuwapandisha mahakamani kwa nguvu watuhumiwa hao akiwemo mwenyekiti Lubongeja aliyesaini mikataba hewa.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2009/10 ni kwamba watumishi 21 katika Halmashauri ya Sengerema wa idara za fedha, manunuzi, elimu, maji, ujenzi, afya na kilimo na mifugo wametajwa kuhusika kutafuna Sh. bilioni 2.5 fedha za miradi ya maendeleo.

Kufuatia taarifa hiyo, Mei 8 mwaka huu, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo, alitoa siku 14 kwa watumishi hao kuandika barua za kujieleza juu ya tuhuma zinazowakabili.

Katika kutekeleza hatua hiyo waliokuwa madiwani wa CCM kata za Nyampulukano, Hamisi Tabasamu na Adrian Tizeba kata ya Lugata baada ya kuhamia Chadema wamesema wako tayari kwenda kutoa ushahidi mahakamani kuhusu namna fedha hizo zilivyotafunwa kutokana na mwenyekiti kushindwa kusimamia vyema majukumu yake.

Kwa upande wake, aliyekuwa mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema, aliwataka wananchi kutambua uthamani wa maisha yao kupinga unyanyasaji na kutoa wito kushikamana katika kupinga hali hiyo.

Katika mkutano huo, Chadema ilivuna wanachama 20 wa CCM waliorudisha kadi zao na kujiunga na Chadema kutoka Katunguru na Sengerema mjini.

Lema yupo kwenye mikutano ya Chadema inayojulikana kama oporesheni ya nchi nzima ya “Vua gamba Vaa Gwanda”

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles