Sunday May 1, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Wananchi walalamikia ukosefu wa dawa za matibabu

12th May 2012
Print
Comments
Mfuko wa Bima ya Afya Taifa

Wakazi  Mkoani Rukwa wamelalamikia ukosefu wa dawa za aina mbalimbali  katika vituo vya kutolea huduma  vya serikali hali inayochangia wao kushindwa kupata msukumo wa kujiunga  na mfuko wa afya ya jamii.

Hayo yalisemwa na baadhi ya wakazi wa kijiji cha Challa kilichopo katika Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa  wakati wakizungumza  na wataalamu  wa Mfuko wa Bima ya Afya Taifa  waliofika katika kijiji hicho kwa lengo la kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii.

Wananchi hao ambao ni Bi Tekra Sangu, pamoja na Bw. Justin Mwanisawa wamesema kumekuwepo na changamoto kubwa ya ukosefu wa dawa katika vituo vya serikali jambo ambalo linalalamikiwa  hasa na wateja wa Bima ya Afya na hivyo kuwafanya waanchi hao kukosa moyo wa kujiunga na mifuko hiyo ya afya ya jamii.

Hata hivyo wananchi hao wamesema kuwa ili mfuko huo uweze kupata wateja wengi serikali iboreshe  hali ya upatikanaji wa dawa katika vituo vya kutolea huduma

Kwa upande wake Meneja  wa Mfuko wa Afya ya jamii Bi Joyce Sumbwe amewataka wananachi  hao kujiunga  na mfuko huo ili waweze kupatiwa huduma za matibabu  bila ya kuwa na fedha mikononi ikiwa ni pamoja na kuufanya mfuko huo uweze kuwa na uwezo wa kupata dawa kwa wingi  kutokana na michango hiyo ya wananchi.

Awali mfuko huo wa Bima ya Afya kabla ya kutembelea  kijiji hicho cha Chala, walifanya mkutano  mkubwa na wadau wa mfuko huo  mjini Sumbawanga  ambapo Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya aliutaka mfuko huo kuboresha huduma za dawa na kuwataka watoa huduma kuwa na lugha nzuri kwa wateja wao.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles