Friday Apr 29, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Kingunge: Wanaoita wenzao mafisadi wamefilisika

7th April 2012
Print
Comments
Mwanasiasa mkongwe nchini Kingunge Ngombale Mwiru

Mwanasiasa mkongwe nchini Kingunge Ngombale Mwiru amesema kuwa viongozi wa dini na wanasiasa wanaowaita wenzao mafisadi ni aina ya viongozi waliochoka na kufilisika.

Akizungumza katika mkutano maalum ulioandaliwa na  CCM Wilaya ya Bagamoyo, Kingunge alisema kuwa viongozi hao wa dini na wanasiasa wanadhani kuwapo kwa mfumo wa vyama vingi na uhuru wa kutoa maoni ni kuruhusu watu kutokua na adabu kwa wenzao.

Alisema kuwa imekuwa ni tabia hivi sasa kwa baadhi ya viongozi wa dini na wanasiasa kutumia majukwaa yao kuwavunjia heshima viongozi waliopo madarakani.

“Hili ni jambo lisilowezekana hata kidogo kiongozi anachaguliwa na wananchi halafu kuna watu wanamvunjia adabu kiongozi huyo huku ni kuwatukana wananchi na hakukubaliki  mahala popote,” alisema Kingunge.

Akuzungumzia suala la ufisadi Kingunge alisema kuwa neno ufisadi maana yake si kama inavyofikiriwa na watu wanaoneza neno hilo bali lina maana mbaya kuliko wanavyolisema baadhi ya watu wakilitumia kuwachafua wenzao.

“Tuache kupakaziana maneno mabaya kama ufisadi kwani neno hilo lina maana mbaya kuliko inavyodhaniwa na iwapo kuna mtu ana ushahidi na matendo ya ufisadi ya mtu ni bora ayatoe hadharani  na kutoa ushahidi kuliko kuendelea kuchafuana,” alisema Kingunge

Akizungumzia masuala ya udini Kingunge alisema kuwa Watanzania wanapaswa kuacha kuendekeza udini kwani baadhi ya wanasiasa na viongozi wa dini ambao wamefilisika kimawazo wamekuwa wakitumia udini kutaka kuwagawa Watanzania.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles