Saturday Apr 30, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Malinzi amwaga fedha kikapu

25th April 2012
Print
Comments
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dioniz Malinzi

Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dioniz Malinzi ametoa fedha zake za mfukoni kwa ajili ya kuwazawadia timu washindi wa kwanza hadi wa tatu wa mashindano ya taifa ya mpira wa kikapu yaliyofikia ukingoni Jumamosi katika uwanja wa ndani wa Taifa.

Akizungumza wakati wa kuwakabidhi fedha hizo, Malinzi alisema wachezaji hao wanastahili pongezi kutokana na kwamba michuano hiyo imeendeshwa bila ya kuwa na mdhamini.

Alisema kama si moyo wa wachezaji wa timu hiyo pamoja na viongozi wa shirikisho la mpira wa kikapu nchini (TBF), wasingeweza kuendelea kushiriki katika mashindano hayo.

"Kwa kweli wachezaji na viongozi wa timu hizi wanastahili pongezi, wameonyesha moyo katika michezo," alisema Malinzi.

Alisema endapo wataendelea na moyo huo, mchezo huo utazidi kukua.

Zawadi ya fedha alizowakabidhi kama motisha ni pamoja na mshindi wa kwanza kwa wanaume timu ya Savio ambao walikabidhiwa medali na fedha taslimu Sh. milioni moja, wakati mshindi wa pili timu ya ABC walikabidhiwa Sh. 500,000 pamoja na medali na wa tatu City Bulls wakipata Sh. 200,000 pamoja na medali.

Kwa upande wa timu za wanawake, vinara Jeshi Stars walikabidhiwa Sh. milioni 1 na medali, Donbosco walioshika nafasi ya pili walipata Sh. 500,000 na medali, wakati Vijana Queens walipata Sh. 200,000 na medali.

Wakati huo huo, Malinzi aliitaka Serikali kuweka juhudi katika michezo, hasa kwa kujenga viwanja ambavyo vimekuwa ni tatizo sugu linalorudisha nyuma maendeleo ya michezo nchini.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles