Thursday Jun 20, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Utoaji fomu Mabwepande wamalizika

24th May 2012
Print
Comments

Zoezi la uchukuaji wa fomu za  ununuzi wa viwanja katika eneo la Mabwe pande jijini Dar es Salaam, limemalizika huku wengi wao wakikosa fomu hizo.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Fortunatus Fwema, azoezi hilo lilimalizika salama ingawa wengi walikosa fomu kutokana na uchache kwa kuwa zilitolewa kulingana na uchache wa viwanja vilivyotangazwa.

Alisema viwanja vilivyotangazwa ni 260, lakini walilazimika kutoa fomu zaidi  ili kuzichambua na kupata watakaokidhi vigezo husika.

Fwema aliongeza kwamba endapo itaonekana waombaji wenye sifa watakuwa wengi na kukosa viwanja katika awamu ya kwanza, watawekwa katika orodha ili wapatiwe katika awamu nyingine.

 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment