



Mchezaji wa kimataifa wa klabu ya Simba Sports ya jijini Dar es salaam Patrick Mutesa Mafisango amefariki dunia alfajiri ya leo kwa ajali ya gari iliyotokea katika eneo la Tazara.
Akizungumza na Radio One Stereo, Mwenyekiti wa klabu ya Simba ambaye pia ni Mbunge wa Tabora Mheshimiwa Ismail Aden Rage ameelezea kupokea kwa masikitiko taarifa hizo.