



Wakati kocha wa mabingwa wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara, Simba, Milovan Cirkovic, akiwa amerejea kwao kwa mapumziko, Mserbia huyo ameacha maagizo kuwa anataka kambi ya timu hiyo ianze mapema kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya Kombe la Kagame yatakayofanyika kuanzia Juni 23 hadi Julai 8 hapa nchini.
Cirkovic ambaye mapema wiki hii alipewa mkataba mpya wa miaka miwili wa kuwafundisha Wekundu hao, ameenda kwao Serbia kwa mapumziko wa wiki mbili.