Saturday May 25, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Karume awafunda wajasiriamali

26th June 2012
Print
Comments
Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume

Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, amewataka wanawake wajasirimali kutengeneza bidhaa zenye viwango vya ubora ili ziweze kuuzika katika masoko kwa wakati ikiwemo kuziongezea thamani.

Aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati akifungua mafunzo ya wanawake wajasiriamali nchini yaliyoandaliwa na Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) ambapo Karume alisema endapo wakilizingatia suala hilo ni kwamba bidhaa zao zitapelekea kuwavutia wateja kwenye masoko na kuzinunua.

Karume alisema katika suala la ushindani huangaliwa bidhaa zenye ubora na hatimaye kupata soko kwa urahisi.

Alisema kuna haja ya wajasiriamali kuweka mkazo katika kuziongezea thamani bidhaa zao kwa lengo la kushindana katika biashara.

“Ukosefu wa masoko ni tatizo kubwa ambalo linawakabili wajasiramali nchini hivyo katika mafunzo hayo mnatakiwa kuwa makini katika kupata mbinu ya kuwapata wateja ili bidhaa zao ziweze kupata masoko,” alisema Karume.

Alisema endapo hawataziongezea thamani bidhaa zao ni kwamba watakuwa wanauza kama malighafi hali ambayo itawasababishia kukosa soka na hata kupata faida kidogo.

Karume aliupongeza mfuko wa EOTF kwa kuandaa mafunzo kwa wanawake ili waweze kupata maendeleo katika masuala ya kiuchumi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa mfuko huo, Mama Anna Mkapa, alisema kupitia mafunzo hayo wakina mama wengi wameweza kupata ujuzi ikiwemo kuziboresha bidhaa zao.

Alisema walioshiriki katika mafunzo hayo ni wanawake 300 na kwamba yanafanyika kutokana na ushindani mkubwa wa kibiashara uliko masokoni.

Alisema kwa mwaka huu wamekuja na mafunzo suluhishi ya kukabiliana na ushindani katika masoko katika kuziongezea thamani bidhaa ili ziwe zinauzika kwa haraka.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment