Saturday May 25, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

UVCCM yajitosa machafuko Z`bar

3rd June 2012
Print
Comments

Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), umejitosa katika machafuko ya Zanzibar ambapo umesema yanasababishwa na vikundi vya mihadhara ya dini kugeuka kuwa vyama vya siasa.

Hayo yalisemwa jana mjini Dodoma na Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM, Benno Malisa, wakati alipokuwa akifungua kikao cha siku mbili cha Baraza Kuu la UVCCM.

Alisema kikao hicho, kitatoa msimamo ni yapi watayafanya katika kuhakikisha kuwa mambo hayo yanamalizika visiwani humo.

“Vuguvugu la kuvunja muungano, kuharibu amani limejitokeza hapa tutatoka na msimamo ni yapi tutafanya kuhakikisha yanafika mwisho...Vikundi vya mihadhara ya dini vimegeuka kuwa vyama vya siasa,” alisema.

Aidha, alisema UVCCM inajipanga kuhakikisha inazima moto wa kisiasa ambao unawashwa na vyama vya upinzani.

Beno alisema mkutano huo ambao unafanyika kikatiba mara moja kwa mwaka utamalizika, vijana watatakiwa kuhakikisha wanajibu mashambulizi ya wapinzani ambao wamekuwa wakizunguka nchi nzima kwa ajili ya kutangaza sera zao ambazo aliziita ni za uongo na uchochezi.

Aidha, Malisa alisema vijana wa CCM wanatakiwa kufanya kazi kwa nguvu kubwa kwani kunyamaza kwao kunatoa mwanya kwa wapinzani kutoa sera zao kwa Watanzania ambazo zimejaa upotoshaji mwingi.

Halikadhalika, Malisa alimpongeza Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Kikwete, kuwapatia vijana nafasi za uongozi pale zinapopatikana.

Awali akaimkaribisha Malisa, Katibu wa umoja huo, Martin Shigela, alisema agenda za kikao hicho ni pamoja na tathimini ya hali ya siasa, mwenendo wa siasa Zanzibar, taarifa ya kamati ya kuhuisha umoja huo inayoongozwa na Hussein Bashe.

Nyingine ni mchakato wa katiba mpya na mchakato wa uchaguzi unaoendelea ndani ya chama na umoja huo.

SOURCE: NIPASHE JUMAPILI
0 Comments | Be the first to comment