


.jpg)
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imesema itatoa hukumu ya kesi inayomkabili aliyekuwa balozi wa Tanzania Rome nchini Italia, Profesa Ricky Costa Mahalu (63) na mwenzake ya kuisababishia serikali hasara ya Euro 2,065,827.60, Julai 11, mwaka huu baada ya pande zote mbili kutoa hoja za kuwatia hatiani washtakiwa au la Juni 11, mwaka huu.
Umauzi huo ulitolewa jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Illivin Mgeta anayesikiliza kesi hiyo.
Hakimu Mgeta alisema Mahakama imeshatoa mwenendo wa kesi kwa pande zote mbili na kwamba watawasilisha hoja za kama mahakama iwatie washtakiwa hatiani au la Julai 11, mwaka huu kwa njia ya maandishi na kesi hiyo itatajwa Juni 14, mwaka huu.