Tuesday May 3, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Udhaifu chanzo cha matumizi mabaya ya ziada serikalini

15th April 2012
Print
Comments
Maoni ya Katuni

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali (CAG) Ludovick Utouh, ametoa ripoti yake ya mwaka wa fedha 2010/2011 ambayo ilikabidhiwa kwanza kwa Rais Jakaya Kikwete halafu ikafikishwa bungeni, ambako CAG pia aliweza kuzungumza na vyombo vya habari kuhusu kilichomo katika ripoti hiyo.

Kimsingi ripoti imeainisha kukua kwa haraka kwa deni la taifa kwa asilimia 38 katika mwaka wa fedha uliopita, halafu matumizi makubwa kuliko makisio katika balozi zetu nchi za nje, kwa kiasi cha sh. bilioni tatu, kuacha posho za maofisa serikalini, pamoja na malipo bila vielelezo vya kutosha. Si masuala mapya.

Mbali na kukua kwa deni la taifa na matumizi yasiyoridhisha, kuna suala la misamaha ya kodi ambayo pia ilipanda kwa kiasi kikubwa (zaidi ya asilimia 40 kwa mwaka huo wa fedha), kukosesha mapato serikali kwa kiasi cha asilimia 2.5 ya pato lote la taifa.

Kwa baadhi ya watu, hali hiyo inaonekana ni uzembe kwa upande wa serikali kuacha mapato makubwa yavuje tu ili kuwaridhisha baadhi ya watu, na kuna wakati (hasa kipindi cha pili cha awamu ya pili), ilikuwa inaelezwa kuwa sababu ya misamaha ni rushwa. Hivi sasa hakuna aliyejitokeza kudai rushwa inachangia kufikiwa misamaha; mingi ni kwa mashirika ya dini.

Wakati balozi za Tanzania nchi za nje zinashutumiwa na CAG kwa matumizi ya ziada tena ya mabilioni, mabalozi wateule waliopangiwa vituo vya kazi na kuapishwa bado baadhi hawajaondoka nchini huku sababu za hapa na pale zikitolewa na wizara . Pengine ni kutokana na ukweli kuwa ikishafikia kiwango fulani cha kukopa katika mabenki ya biashara na Benki Kuu, inafikia mahali mikopo haiwi rahisi tena kupatikana, na mafungu ya ziada ya mapato kulinganisha na bajeti au mikopo hayapo.

Inabidi serikali ingoje mwaka wa fedha mpya uanze ili iingize matumizi ya muda wa lalasalama wa mwaka wa fedha uliotangulia kama kipaumbele; hasa ni suala la uwajibikaji .

Ukiangalia yaliyomo katika ripoti hiyo na yaliyojiri katika mkutano wa hivi karibuni na Tume ya Umoja wa Afrika ya utawala bora, unakuta kuwa udhaifu uko maeneo mawili, lakini uwajibikaji pia upo.

Kwa maana hiyo Tanzania ina matumizi mabaya ya fedha lakini kwa vile kwa jumla serikali inakubali uwajibikaji kwa ndani (kwa mfano ripoti hiyo ya CAG na kujibu maswali ya tume hiyo ya utawala bora), bado hali siyo mbaya sana.

Inapofikia mahali ambapo serikali haitaki hata kujibu maswali kuhusu matumizi yake, ni wazi kuwa msingi wa uelewano na demokrasia upo mashakani; ina maana hali iliyopo inarekebishika.

Moja ya sababu za matumizi yanayozidi ni kuwa mwaka wa fedha wa 2010/2011 ulikuwa pia mwaka wa uchaguzi mkuu, ambako kunakuwepo sababu kubwa ya kupendeza makundi tofauti ya watu. Matokeo yake ni kutoa misamaha ya kodi, kuruhusu idara tofauti kufanya ununuzi ambao haukupangiwa bajeti, na kuahirisha ‘maamuzi magumu’ ambayo hayafurahishi baadhi ya makundi ya jamii.

Moja ya mbinu za kufuta sehemu kubwa ya deni la serikali na kupunguza mzigo wa ruzuku ni ubinafsishaji wa mashirika ya umma yasiyo na tija kama Air Tanzania, Tanzania Railways, Tanesco, NIC na mengineyo.

Lakini jaribu kuwaambia wanaharakati uone. Majuzi wamemwita UDSM Rais Mstaafu Benjamin Mkapa ‘ili kuhoji sera zake za ubinafsishaji na utandawazi,’ kwani hawaoni faida zake. Je, maudhui ya jambo hili yakoje? Yafaa sote tutafakari mambo haya ili sote kama taifa jujiweke imara katika kupigania mustakabali wa nchi yetu.

SOURCE: NIPASHE JUMAPILI
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles