Friday May 6, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Ulimwengu atua, U-20 yakamilika

17th April 2012
Print
Comments
Thomas Ulimwengu

Kikosi cha timu ya soka ya taifa ya vijana wa umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes), jana kilikamilika baada ya wachezaji wake kadhaa kuripoti kwenye kambi hiyo akiwemo, Thomas Ulimwengu, aliyewasili nchini juzi akitokea mjini Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Awali Ulimwengu anayeichezea TP Mazembe alitarajiwa kuwasili nchini Jumamosi lakini ilishindikana kutokana na kuchelewa ndege na hivyo juzi alifanikiwa kuanza safari na usiku aliripoti kwenye kambi ya timu hiyo.

Wachezaji wengine yosso ambao walikuwa wanamuumiza kichwa kocha wa timu hiyo Kim Poulsen ni Hassan Dilunga kutoka Ruvu Shooting, Issa Rashid na Kesi Khamis wa Mtibwa Sugar ambao nao jana asubuhi walianza mazoezi na kikosi hicho cha taifa.

Dilunga, Rashid na Khamis walikuwa wanazitumikia klabu zao katika mechi za ligi za kuu ya Bara zilizochezwa mwishoni mwa wiki.

Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, alisema kuwa jana asubuhi timu hiyo ilikuwa imekamilika na wanatarajia Kim ataweza kuendelea vizuri kuwanoa wachezaji wake ili kujiandaa na mechi yao ya Jumamosi dhidi ya yosso wenzao wa Sudan.

Yosso hao wa Tanzania na Sudan watakutana katika mchezo wa awali wa kuwania tiketi ya kufuzu kucheza fainali zijazo za vijana za Afrika ambazo zitafanyika baadaye mwaka huu nchini Algeria.

Kwa mujibu wa wasimamizi wa mashindano hayo Shirikisho la Soka la Afrika (CAF), timu nne zitakazofanya vizuri kwenye fainali hizo zitapata tiketi ya kuiwakilisha Afrika kwenye mashindano ya dunia ya vijana.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles