Friday Apr 29, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

`Watimueni wabunge waliowatelekeza’

8th May 2012
Print
Comments

Wanazuoni waliopo katika mikoa ya Njombe na Iringa wameungana na asasi za kiraia katika ukanda huo wameapa kuwa  watatumia taaluma na nafasi zao kuwashawishi wananchi wawafukuze majimboni wabunge wao waliohamishia makazi yao nje ya jimbo na kuwatelekeza wananchi baada ya kuchaguliwa.

Aidha, wamewataka wananchi kuchukua hatua hiyo dhidi ya wabunge wote ambao hawafiki majimboni kusikiliza kero zao na kutoa visingizio visivyokwisha kwamba wametingwa na majukumu ya kitaifa ikiwemo kuwa mawaziri.

Walitoa angalizo hilo jana katika mdahalo kuhusu utawala bora, mchakato wa katiba mpya na wajibu wa viongozi wa kisiasa kwa wananchi. Mdahalo huo uliandaliwa na mtandao wa mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani Njombe maarufu kama Njodingo.

Mitandao hiyo imepanga kuwashawishi wananchi kuwafukuza majimboni wabunge wanaochapa usingizi bungeni, wanaoshabikia hoja ya posho, walioshindwa kutekeleza ahadi zao.

Miongoni mwa wasomi waliozungumza ni Mhadhiri Mwandamizi wa Kitivo cha Uchumi na Biashara wa Chuo Kikuu cha Tumaini mkoani Iringa, Dk. Bukaza Chachage; Mtaalamu wa masuala ya viwango mkoani Njombe, Muhema Olafu na mwanasheria wa kujitegemea, Alatanga Nyagawa,

“Tunataka katiba tunayoiandaa hivi sasa ieleze wazi kwamba mbunge atakayeshindwa kutimiza wajibu wake ikiwemo kuishi jimboni, kutekeleza ahadi zake kwa wakati, kuchapa usingizi bungeni na kuendekeza hoja ya posho wakati wananchi wana matatizo, wananchi wapewe meno kikatiba ya kumtimua kabla ya kufikisha miaka mitano,” alisema Dk. Chachage.

Dk. Chachage alisema wananchi wanapaswa kuacha kulalamika, badala yake wanatakiwa kuwaeleza wabunge hao kwamba ubunge ni mali ya wananchi na uwaziri ni wa kwake, hivyo mbunge anatakiwa kuwatumikia wananchi jimboni kwake kama alivyoomba wakati wa uchaguzi.   

“Huyo mliyemchagua akija jimboni halafu anajitetea kwamba yeye ni waziri na ametingwa na majukumu ya kitaifa, mwambieni uwaziri ni wa kwako na huu ubunge ni wa kwetu, kwa hiyo tunataka ututumike kama ulivyoomba wakati wa uchaguzi...maana kuongoza ni kuwafanya wengine watende kwa kuamini,kukubali na kuridhika,” alisema Dk. Chachage.


SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles