Sunday May 1, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Mali za viongozi 141 zahakikiwa

9th May 2012
Print
Comments

Viongozi wa umma 141 wamehakikiwa mali zao ili kubaini kama kulikuwa na udanganyifu wakati wakijaza fomu za mali wanazomiliki pamoja na madeni yao.

Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Afisa Habari wa Sekretarieti  ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Johanither Barongo.

“Mwaka jana tulikuwa na zoezi la kuhakiki mali za viongozi wa umma na tumefanya kazi hiyo kwa kanda sita,” alisema Barongo.

Alisema zoezi hilo lilikwenda vizuri na kwamba muda wowote watatoa kwa umma ripoti ya uhakiki huo.

Hata hivyo, Barongo hakutaka kuingia kwa undani juu ya matokea ya zoezi hilo na kusema kuwa kila kitu kitawekwa wazi kwa umma baada ya ripoti ya pamoja kukamilika.

Alifafanua kuwa katika zoezi hilo sio viongozi wote wa umma waliohakikiwa, bali walichagua baadhi na kwamba hawakupata kikwazo chochote wakati wa zoezi hilo.

“Hatukupata kikwazo, tulipata ushirikiano wa kutosha katika maeneo yote tuliyopita na watu wote tuliozungumza nao,’’ alisema.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles