Saturday Feb 13, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Ngorongoro yasonga mbele Afrika

7th May 2012
Print
Comments
Timu ya Ngorongoro Heros

Goli pekee lililofungwa na mashambuliaji wa timu ya soka ya vijana ya Tanzania ya umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes), Thomas Ulimwengu, katika dakika ya 12 liliipa nafasi timu hiyo kusonga mbele katika mashindano ya vijana ya Afrika licha ya kufungwa na wenyeji Sudan magoli 2-1 katika mechi yao ya marudiano iliofanyika juzi kwenye Uwanja wa Khartoum nchini humo.

Katika mchezo wa kwanza uliofanyika hapa nyumbani Ngorongoro Heroes ilishinda magoli 3-1 hivyo imesonga mbele kwa jumla ya magoli 4-3.

Kutokana na matokeo hayo sasa Ngorongoro itawakaribisha yosso wenzao kutoka Nigeria Julai 28 hapa nchini na kurudiana nao mapema mwezi Agosti mwaka huu.

Wenyeji Sudan ndio walikuwa wa kwanza kupata goli kwenye mchezo huo wa juzi katika dakika ya 10 kupitia kwa Mohammed Abderahman ambapo dakika mbili zilizofuata ndipo Ulimwengu anayechezea klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) alipowanyanyua Watanzania kwa kufunga goli lililowafanya waende mapumziko wakiwa sare ya 1-1.

Ahmed Nasr aliipatia Sudan goli la pili kwa njia ya penati katika dakika ya 65 lakini halikutosha kuifanya timu hiyo isonge mbele kwenye mashindano hayo ya Afrika mwaka huu.

Kikosi cha kwanza cha Ngorongoro Hereos kilichoanza katika mchezo huo kilikuwa : Aishi Manula, Ramadhan Khamis, Issa Rashid, Samir Ruhava, Dizana Ramadhan, Frank Damayo, Frank Sekule, Omega Seme, Ulimwengu, Simon Msuva na Ramadhan Singano 'Messi'.

Yosso hao wa Tanzania wanaofundishwa na Kim Poulsen walitarajiwa kurejea nchini jana jioni.

Mwaka jana katika kusaka tiketi ya kucheza fainali za Olimpiki, timu ya vijana ya Tanzania ya umri chini ya miaka 23 iliyokuwa chini ya Jamhuri Kihwelu 'Julio' ilitolewa na wenzao wa Nigeria hivyo Ngorongoro Heroes inatarajia pia kukutana na upinzani kutoka kwa wapinzani hao.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment