Friday May 6, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Jalada la yaya anayedaiwa kuua mtoto kwa AG

25th May 2012
Print
Comments

Jalada la kesi ya mauaji ya mtoto Angel  (miezi nane), yaliyodaiwa kufanywa na msaidizi wa kazi za nyumbani, Marieta Petro (17), linatarajia kutinga leo kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kwa ajili ya kuandaa mashitaka.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, John Mtarimbo, alithibitisha hayo jana jijini Dar es Salaam alipozungumza na gazeti hili.

Kamanda Mtarimbo alidhibitisha polisi kumshikilia mtuhumiwa huyo na kueleza kuwa, wakati wowote kuanzia leo watalipeleka jalada la kesi hiyo kwenye ofisi ya AG kwa ajili hatua nyingine za kisheria.

Msichana huyo alikamatwa Jumatano iliyopita eneo la Mwananyamala na wazazi wa marehemu Angel  baada ya kumuona akipita eneo hilo.

Baada ya kukamatwa wazazi hao walimchukua hadi nyumbani kwao, eneo la Sinza Africa Sana ambapotafrani kubwa iliibuka kutokana na wakazi wa eneo hilo kutaka kumpiga, lakini alinusurika kwa kufungiwa ndani.

Kifo cha mtoto huyo kilitokea Machi mwaka huu muda mfupi baada ya wazazi hao kwenda kazini na kumuacha msichana huyo na marehemu Angel.

 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles