Friday May 24, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Watoto wa mitaani waipasua kichwa serikali

15th May 2012
Print
Comments
Naibu Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu

Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, imeandaa mpango mkakati utakaosaidia kupunguza tatizo la watoto wa mitaani hapa nchini.

Hayo yalielezwa jana na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Ummy Mwalimu, alipokuwa akitoa taarifa ya Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, kuhusu maadhimisho ya siku ya Familia Duniani yanayofanyika leo.

Alisema siku hii ambayo huadhimishwa Mei 15 kila mwaka na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kwa mujibu wa Tamko na.47/237 la Umoja wa Mataifa la mwaka 1993, itaadhimishwa na Watanzania kimkoa, ikiongozwa na kauli mbiu ya, “Uwajibikaji Sawa katika Majukumu, Msingi wa Familia Bora”.

Mwalimu alisema kauli mbiu hiyo inaikumbusha jamii kuthamini utamaduni wa kuendeleza mfumo wa familia tandaa, kama ilivyokua hapo zamani ili kusaidia kupunguza tatizo la watoto wa mtani.

“Kudhoofika kwa utamaduni wa zamani wa kuenzi mfumo wa familia tandaa, ambapo ndugu na jamii walikuwa wakisaidiana katika malezi ya watoto, kunachangia ongezeko la watoto wa mtaani na wanaoishi katika mazingira magumu,” alisema.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment