Thursday Jun 20, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Yanga watinga bungeni na Kombe la Kagame leo

6th August 2012
Print
Comments
Mabingwa wa soka wa Afrika Mashariki na Kati, Yanga

Mabingwa wa soka wa Afrika Mashariki na Kati, Yanga wataonyesha kombe lao la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame)  ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo wakati watakapotembelea kwa mwaliko wa wabunge walio na unachama wa klabu hiyo ya ‘Wanajangwani’.

Akizungumza jijini Dar es Salaam kabla ya timu yao kuondoka jana kuelekea Dodoma, Afisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu, alisema kuwa wamefurahi kupata mwaliko wa kwenda tena bungeni kutoka kwa wabunge walio wanachama wa klabu yao, kama ilivyokuwa mwaka jana wakati walipotinga bungeni pia baada ya kulitwaa taji la michuano hiyo kwa kuwafunga watani zao wa jadi, Simba.

Wiki iliyopita, Yanga walitwaa ubingwa wa Kagame kwa mara ya pili mfululizo baada ya kushinda 2-0 katika mechi yao ya fainali dhidi ya Azam kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

"Tumefurahi kupata mwaliko wa kwenda bungeni (na kombe), tunakwenda huku tukiwa na furaha zote za kuibuka na ushindi," alisema Sendeu.

Wabunge walio wanachama wa Yanga wameialika timu hiyo bungeni ikiwa ni siku chache tu baada ya kuzindua tawi la klabu hiyo bungeni linaloongozwa na Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Mhe. Mohamed Misanga na katibu wa tawi hilo ni Mbunge wa Mbozi Mashariki, Mhe. Godfrey Zambi.   

Sendeu aliwataja baadhi ya wachezaji watakaolitambulisha kombe la Kagame bungeNI leo kuwa ni Yaw Berko, Ali Mustafa 'Barthez', Said Bahanunzi, Hamisi Kiiza, Nurdin Bakari na Rashid Gumbo.

Wengine ni Haruna Niyonzima, Athuman Idd 'Chuji',  Godfrey Taita, Seif Kijiko, Simon Msuva, Ali Shamte, Jerryson Tegete, Kelvin Yondani, Nadir Haroub Canavaro na Nizar Khalifan.

Katika hatua nyingine, Sendeu aliongeza kuwa baada ya kurejea kutoka bungeni, wataendelea na mazoezi chini ya makocha wao Tom Santief na Fredy Felix Minziro kujiandaa na ligi kuu ya Tanzania Bara itakayoanza mapema mwezi ujao.











 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment