Saturday May 18, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Wizara ya habari yakanusha kuwepo mgogoro

9th June 2012
Print
Comments
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Seth Kamuhanda

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Seth Kamuhanda amekanusha kuwepo na mgogoro ndani ya Wizara hiyo kati yake na waziri wake Dk. Fenella Mukangara.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu huyo alisema kutokana na uadilifu na umakini wa utendaji kazi wa Waziri wake kamwe haitakuwa rahisi mtu kumuwekea vipingamizi au kujenga naye migogoro.

Hata hivyo, katika mkutano huo na waandishi, Kamuhanda alikuwa peke yake kitendo ambacho kiliongeza kuwepo na hali ya wasiwasi juu ya mahusiano ya viongozi hao wakuu wa Wizara hiyo. 

NIPASHE ilipofanya juhudi ya kumtafuta Waziri Mukangara kwa njia ya simu ili aweze kuzungumzia tamko hilo, alipokea kisha kukata simu na alipopigiwa kwa mara nyingine hakupokea.

Katibu huyo, alisema taarifa iliyotolewa na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) haikuwa na ukweli wowote na kwamba kilichoelezwa na Wahariri hao ni hisia baada ya wao(viongozi wizarani) kukosekana kwenda kufungua na kufunga mkutano wa mashauriano kati yao na Baraza la Habari (MCT) uliofanyika mjini Morogoro.

Alisema sababu kubwa iliyowafanya kutokwenda katika mkutano huo ni kuzidiwa na maandalizi ya vikao vya Kamati ya Bunge, ambapo yeye na waziri ndio wahusika wakuu wa vikao hivyo.

Kamuhanda alisema licha ya kukabiliwa na vikao hivyo, alitoa taarifa kwa Baraza la Habari, ambapo kwa namna isiyofahamika wahusika hawakuweza kutoa taarifa za kutofika kwao katika mkutano huo.

"Katika mkutano ule ambao sote tulipenda kuhudhuria na kuongea na Wahariri tulishindwa kuhudhuria kutokana na kukabiliwa na vikao vya kamati za  bunge, hata hivyo tulitoa taarifa MCT lakini nashangaa pale ninapoelezwa hawakuwa na taarifa yoyote," alisema Kamuhanda

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment