Thursday May 5, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Mtanzania afika kileleni mlima Everest

21st May 2012
Print
Comments

Wilfred Moshi mkazi wa Shirimatunda Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, ameweka historia kwa kuwa Mtanzania wa kwanza kufika kwenye kilele cha mlima Everest nchini Nepal, baada ya safari ya mwezi
mmoja na nusu, kwa kufanya mazoezi na kisha kwenda kileleni.

Akizungumza na NIPASHE kwa njia ya Mtandao alisema safari ya kwenda kileleni waliianza Mei 15, Mwaka huu, ambapo Mei 19, mwaka huu majira ya saa 3 asubuhi alifanikiwa kuwa kwenye kilele cha mlima huo na kuweza kupeperusha bendera ya Tanzania.

Awali, akiongea na NIPASHE akiwa kwenye urefu wa mira 7,200 kutoka usawa wa bahari, alisema ni kazi ngumu sana yenye kuhitaji uvumilivu na jitihada binafsi na alikuwa na matumani makubwa ya kufika kwenye kilele cha mlima hyuo.

Moshi alisema kupanda mlima huo kunahitaji vifaa na ujuzi hivyo muda mwingi wanatumia katika kujifunza kabla ya kuanza safari ya kwenda kileleni.

“Unatakiwa ujue jinsi ya kupanda kwenye kuta za barafu kwa kutumia viatu vyenye soli ya chuma kwa kutumia kamba hadi sasa nimeweza kupanda mita 7,200 kutoka usawa wa habari kwa ajili ya mazoezi tu”
alisema.

Alisema hadi sasa afya yake ni nzuri ila amepungua uzito kwa kiasi kikubwa kutokana na kukaa kwa muda mrefu usawa wa juu wa bahari na kwamba kwenye kupanda mlima huo kunategemea hali ya hewa ikoje na muda wote wanaangalia kwenye kompyuta zilizoungwanishwa na mtandao
kujua hali ya hewa ikoje ili kuweza kuendelea na safaru au la.

“Nawashukuru sana Watanzania wenzangu kwa sala zao za hali na mali sasa nimeweza kuipeperusha bendera ya nchi yangu na kuitangaza nchi yangu, najivunia sana kuwa Mtanzania, ni matumaini yangu kuwa serikali itatambua na kuthamini mchango wangu,” alisema.

Wilfred ni miongoni mwa kundi la watu watano kutoka nchi za Finland, Uingereza, New Zealand na Spain, ambao pamoja na malengo mengine walipanda mlima huo kwa lengo la kuanzisha Shirika lisililo la
kiserikali litakaloitwa Twende Pamoja (Hand by Hand Cloba Vision Project), litakaloanzishwa mjini Moshi, ambapo pamoja na Wilfred wengine wawili walifika kileleni pia.

Aidha, akifananisha na eneo la Sado ambalo ni gumu sana kwenye kupanda Mlima Kilimanjaro huko lipo eneo liitwalo Papcorn na Ice Fall ambayo hutokea maporomokoo ya barafu mara kwa mara, ambapo hutakiwi kukaa bali kupita kwa haraka na alimudu kufanya hivyo.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles