Wednesday May 4, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Twiga Stars wajazwa noti

25th May 2012
Print
Comments
Timu ya Soka ya Taifa ya Wanawake Twiga Stars

Kocha wa timu ya soka ya taifa ya wanawake (Twiga Stars), Boniface Mkwasa, amesema kuwa timu yake inakwenda Addis Ababa nchini Ethiopia kupambana ili wapate ushindi na mashabiki wa timu hiyo wasiwe na hofu licha ya kikosi chake kufanya vibaya kwenye mechi za kirafiki za kimataifa walizocheza hivi karibuni.

Twiga Stars iliondoka nchini jana jioni kuelekea Ethiopia kuwavaa wenyeji wao katika mechi ya kwanza ya kuwania tiketi ya kucheza fainali zijazo za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake.

Akizungumza jana mchana baada ya kukabidhiwa bendera, Mkwasa, alisema kuwa timu yake imefanya mazoezi kwa siku 34 kujiandaa na mechi hiyo na tayari amerekebisha makosa yaliyojitokeza na anaamini wakiwa Ethiopia watakuwa makini na hatimaye kurejea nyumbani na ushindi.

Mkwasa alisema kuwa amekiimarisha kikosi chake vizuri katika kila idara kwa sababu wanawafahamu wapinzani wao ni wazuri na waliwasumbua mara ya mwisho walipokutana mwaka 2010.

"Tumeufanyia kazi udhaifu uliokuwepo, tumejiandaa kuleta faraja, heshima ya nchi na sisi wenyewe," alisema kocha huyo ambaye pia aliiongoza Twiga Stars katika fainali zilizopita.

Nahodha wa Twiga Stars, Asha Rashid 'Mwalala', alisema kuwa wachezaji wamejiandaa vyema ili kuhakikisha wanafanya vizuri na kurejea nyumbani wakiwa na ushindi.

Akikabidhi bendera ya taifa, Naibu Waziri, Wizara ya Habari, Ajira, Utamaduni na Michezo, Amos Makala, aliwataka wachezaji wakaingie uwanjani kwa lengo moja la kusaka ushindi na kulinda mafanikio waliyonayo.
 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles