


.jpg)
Serikali bado haijatekeleza tamko la Chama cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (Trawu) la kuwalipa wafanyakazi wake mishahara ya Machi na Aprili, mwaka huu.
Akizungumza na NIPASHE jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Trawu, Erasto Kihwele alisema kuwa wafanyakazi wote wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (Tazara) hawajalipwa mishahara yao kwa kuwa hata serikali bado ipo kimya kuhusu hilo hivyo haifahamiki ni lini mishahara hiyo italipwa.
“ Tatizo hili ni kubwa kwani kila mfanyakazi hutegemea kulipwa mshahara wake kila mwisho wa mwezi, lakini ikiwa ni kinyume chake huleta migogoro sehemu ya kazi kwa kuwa Waziri alitusihi kutofanya chochote hadi tuonane naye hivyo kimya chao kitafahamika,” alisema.
Awali Trawu ilitoa tamko na kuipa Serikali siku tano kuwalipa wafanyakazi wake mishahara kutokana na uongozi wa Tazara kushindwa kutekeleza ahadi yao waliyoitoa mbele ya Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu.
Kihwele alisema kuwa Ijumaa iliyopita walikwenda kuonana na Nundu ili kujua hatma ya mishahara yao, lakini Waziri alikuwa Mkoani Tanga, hivyo leo watakwenda kuonana naye.