Sunday May 1, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Mengi kutumukiwa tuzo ya Amani katika Biashara

3rd May 2012
Print
Comments
Rais wa Chama Cha Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo, Alloyce Mwamanga (katikati), akizungumza na waandishi wa habari juu ya Tuzo ya Amani katika Biashara atakayotunukiwa Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dk. Reginald Mengi, katika sherehe itakayofanyika Oslo nchini Norway Jumatatu ijayo.

Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dk. Reginald Mengi, anatarajiwa kutunukiwa tuzo ya Amani katika Biashara (Business for Peace Award) ya mwaka 2012, Mei 7 mwaka huu, mjini Oslo, Norway.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Rais wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA), Aloys Mwamanga, alisema chama chake kwa kushirikiana na Jumuiya ya Kimataifa ya Wafanyabiashara (ICC), watatoa tuzo hiyo.

Alisema tuzo hiyo ambayo ni ya kwanza kwa Tanzania, hutolewa kwa mfanyabiashara anayefanya biashara kwa utaratibu unaotakiwa ulimwenguni na aliyejitoa kutatua matatizo ya watu wanaoishi katika mazingira anayofanyia kazi.

“Ili kuwa mshindi lazima mhusika awe mfano wa kuigwa kwa kutoa ajira kwa watu walioko kwenye mazingira ya biashara yake pamoja na kutatua matatizo mbalimbali ya watu hao,” alisema Mwamanga.

Mwamanga alisema TCCIA ilipata nafasi ya kutoa majina ya wafanyabiashara watano toka Tanzania, ambapo Dk. Mengi aliibuka mshindi kati ya wafanyabiashara wakubwa 90 kutoka katika nchi zaidi ya 60 duniani.

Aidha, alisema katika Bara la Afrika ni mara ya tatu kupata tuzo hiyo, ambapo alitaja nchi nyingine zilizowahi kupata tuzo hiyo kuwa ni Nigeria na Uganda.

Mkurugenzi wa TCCIA, Daniel Machemba, aliwataka wafanyabiashara wengine kujitolea kutatua matatizo ya wananchi wanaoishi katika mazingira yao ya kazi ili nao wapate nafasi hiyo. “Mengi hajapewa kwa sababu yeye ni tajiri sana, lakini ni kutokana na kujitolea kusaidia wananchi waliopo kwenye mazingira yake ya kazi,” alisema Machemba.

Aliwataja washindi wengine kutoka nchi mbalimbali watakaopewa tuzo hiyo, kuwa ni Ibrahim Abouleish (Misri), Anil Agarwal ( India) na Eduardo Eurnekian (Argentina).

Wengine ni Vladas Lasas (Lithunia), David  MacLennan (Marekani) pamoja na Latifur Rahman (Bangladesh).

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles