Tuesday May 21, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Omar Kapera apata ahueni, mtoto wake afafanua

3rd July 2012
Print
Comments
Taifa Stars

Hali ya kiafya ya gwiji wa zamani wa soka nchini aliyewahi kutamba na klabu za Yanga, Nyota Afrika, Pan African na Taifa Stars, Omar Kapera 'Mwamba' inaendelea kutengemaa.

Mtoto wa mkubwa wa beki huyo wa zamani anayesumbuliwa na ugonjwa wa kupooza, Mohammed Kapera, amefafanua kwamba baba yake hahitaji kuchangiwa kitu chochote kwa sasa kwani wanamsaidia vya kutosha.

Kapera aliyekumbwa na kiharusi miezi nane iliyopita alisema hali yake kwa sasa inaendelea vema na anamshukuru Mungu, lakini amewasihi Watanzania wazidi kumuombea apone haraka ili aendelee na kazi za ujenzi wa taifa.

"Namshukuru Mungu naendelea vema, kila siku zinavyosonga mbele hali inatia matumaini, lakini nawaomba Watanzania waniombee zaidi," alisema mkongwe huyo aliyewahi kuwa Afisa Michezo na Katibu Mkuu wa klabu ya Pan.

Kapera alisema anashukuru hali ya mzee wake inaendelea vema na amesisitiza kuwa hahitaji kuchangiwa.

"Watu wasisumbuke kumchangia baba yetu, sisi tunamudu kumtunza, zaidi wamuombee dua na kumpa pole tu, sio kumchangia chochote hahitaji kwa sasa namba iliyotolewa ni kwa ajili ya kumjulia hali tu," alisisitiza Kapera.

NIPASHE liliripoti wiki iliyopita juu ya afya ya mchezaji huyo, ambapo gwiji huyo aliridhia kutoa namba yake ili wanaohitaji kumpa waitumie, jambo linalodaiwa limekuwa kero ndio maana mtoto huyo ameamua kutoa ufafanuzi.

 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment