Sunday May 1, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Madaktari kukutana keshokutwa

24th May 2012
Print
Comments

Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) kimetangaza kusudio la madaktari wa kada zote kukutana kwenye mkutano Juni 2, utakaofanyika jijini Dar es Salaam.

Taarifa ya MAT iliyotolewa kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana ilieleza kwamba lengo kuu la Mkutano huo ni kutoa taarifa ya mrejesho juu ya mambo yaliyokuwa yakijadiliwa kati ya wawakilishi wa madaktari na Serikali kupitia Kamati ya majadiliano juu ya madai ya madaktari.

"Tumeona wakati majadiliano yakiendelea ni wakati muafaka kwa taarifa hizi za majadiliano kuwafikia madaktari ili nao wapate nafasi ya kusikia, kujadili na kutoa mapendekezo ya nini kinapaswa kufanyika ili kufikia mahala bora zaidi kwa maslahi ya afya ya Watanzania na Nchi kwa ujumla," alisema.

Taarifa hiyo haikueleza ukumbi utakakofanyika mkutano huo na badala yake MAT imeeleza kwamba itautangaza badae

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles