Thursday May 5, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Mfumuko wa bei wapungua, Shilingi yaporomoka

16th May 2012
Print
Comments

Mfumuko wa bei kwa mwezi Aprili umepungua kutoka asilimia 19.0 Machi hadi kufikia asilimia 18.7 huku thamani ya Shilingi ya Tanzania ikiendelea kuporomoka.

Taarifa ya kila mwezi ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), inaonyesha kwamba thamani ya fedha ya Tanzania imeendelea kuporomoka thamani kutokana na gharama za bidhaa kupanda kila wakati.

"Thamani ya Shilingi ya Tanzania inapima badiliko la uwezo wake katika kununua bidhaa na huduma zilezile za mlaji ambazo Shilingi ya Tanzania itaweza kununua katika vipindi tofauti, ikiwa wastani wa farihisi za bei za taifa unaongezeka, thamani ya fedha hupungua," ilieleza sehemu ya taarifa ya NBS iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa ofisi hiyo.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa bei za vitu mbalimbali zimeongezeka kutokana na kupanda kwa bei za vyakula, vinywaji baridi, nishati na mafuta.

Ilieleza kwamba kwa kipindi cha Aprili mwaka jana hadi Aprili mwaka huu, bidhaa hizo zimekuwa na mwenendo wa bei usio imara ikilinganishwa na bidhaa nyingine.

Hata hivyo, taarifa hiyo ilifafanua kuwa mfumuko wa bei za nishati umepungua kutoka asilimia 29.4 Machi hadi asilimia 24.9 Aprili.

Kwa upande mwingine, ilieleza kuwa mfumuko wa bei ambao haujumuishi vyakula na nishati imeongezeka hadi asilimia 9.0 Aprili, kutoka asilimia 8.8 Machi.

Iliongeza kuwa bei za vyakula vimechangia mfumuko wa bei ikiwemo mchele ambao umeongezeka kwa asilimia 3.0 na unga wa mahindi kwa asilimia 0.5.

Baadhi ya vyakula vingine vilivyoongeza mfumuko wa bei na asilimia zake kwenye mabano ni punje za mahindi (1.6), vitafunwa (7.3), unga wa mihogo (6.7), mayai (2.1), siagi (2.9), machungwa (6.8) na maembe (12.8).

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles