Tuesday May 3, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Ngeleja atunukiwa hati maalum ya shukrani

10th May 2012
Print
Comments
Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Wiliam Ngeleja.

Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu  ya Chama cha Mapinduzi(CCM) Wilaya ya Sengerema, Mkoani Mwanza, imemtunuku hati maalumu ya shukrani, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Wiliam Ngeleja.

Aidha, Chama cha Mapinduzi Wilayani humo kinaandaa mapokezi makubwa pamoja na maandano ya kumpokea Ngeleja atakapokwenda jimboni humo hivi karibuni, ikiwani siku cahche baada ya kuachwa katika Baraza la Mawaziri lililotangazwa hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete.

Hati hiyo ilikabidhiwa kwa Katibu wa Mbunge huyo, Peter Ngelela kwa niaba ya Ngeleja ambaye ni Mbunge wa Sengerema, jana wakati wa kikao cha wajumbe  wa halmashauri kuu ya chama wilaya.

Akizungumza kabla ya kuikabidhi hati hiyo, Katibu wa CCM  Wilaya ya Sengerema, Magdalena Ndwete, alisema Ngeleja amekuwa mstari wa mbele kukisaidia chama (CCM) na jumuia  zake zote tangu achaguliwe kuwa mbunge jimbo jilo mwaka 2005.

"Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi wilaya inatambua na kuthamini mchango mkubwa wa hali na mali wa Mheshimiwa Wiliam  Mganga Ngeleja kusaidia chama na jumuia zake tangu achagulilwe kuwa Mbunge wa Jimbo la Sengerema" alisema Ndwete na kuongeza kwamba:

"Amekuwa mstari wa mbele kusaidia Chama cha Mapinduzi na jumuia zake pindi anapopewa taarifa ya kufanya hivyo".

Aliyataja baadhi ya mambo yaliyofanywa na Ngeleja wilayani humu kuwa ni, kuiwezesha CCM na jumuia zake kufanya ziara katika kata zote pamoja na matawi yote kuimarisha chama tangu alipochaguliwa kuwa mbunge.

Katibu huyo  aliyataja mambo mengine yaliyofanywa na Ngeleja kwamba ni utekelezaji mzuri  wa Ilani  ya Uchaguzi ya CCM katika jimbo la Sengerema; hali ambayo imekisaidia chama hicho kuendelea kupendwa  na wananchi pamoja  na kuendelea kuwa na imani nacho.

Alisema Ngeleja pia amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba CCM na jumuia zake wilayani  humo hakikwami  katika kuendesha  shughuli zake za kila siku.

Mbali na Katibu huyo, baadhi ya wana-CCM walijitokeza kuunga mkono  uamuzi wa Kamati ya Siasa ya  Halmashauri Kuu  ya  Wilaya ya Sengerema  kwa uamuzi huo  wa kumtunuku Ngeleja, kwani pia amesababisha Jimbo la Buchosa kupata nishati ya umeme.

Wakati huohuo, Ngelela, alisema ofisi yake inaandaa mapokezi makubwa ya kumpokea Ngeleja ambaye anatarajiwa kuwa jimboni humo siku yoyote mwezi huu.

Alisema ofisi yake imeshaanza mchakato  kwa ajili ya kufanikisha maandamano hayo,  ambayo alisema yatakuwa ya kihistoria wilayani humo.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles