Tuesday Feb 9, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

EAPCCO yafuatilia utekelezaji wa polisi

17th April 2012
Print
Comments

Jeshi la Polisi la Tanzania limekuwa mwanachama wa kwanza kati ya wanachama wa Jumuiya ya Wakuu wa Majeshi ya Polisi ya Nchi za Afrika Mashariki (EAPCCO), kufuatiliwa kuona lilivyotekeleza maazimio ya jumuiya hiyo, ikiwamo udhibiti wa wizi wa fedha kwa kutumia mtandao wa kompyuta.

Mazimio mengine yaliyopitishwa na mkutano wa EAPCCO uliofanyika mjini Kigali, Rwanda, mwaka jana, ni pamoja na udhibiti wa uhamiaji haramu na dawa za kulevya.

Mengine ni vitendo vya utakatishaji wa fedha haramu na namna Jeshi la Polisi la Tanzania lilivyojiandaa kwa ajili ya mazoezi ya pamoja ya siku tano yanayotarajiwa kufanyika Agosti, mwaka huu, mjini Kigali.

Mwenyekiti wa EAPCCO ambaye ni Mkuu wa Jeshi la Polisi la Rwanda, Inspekta Jenerali (IGP), Emmanuel Gasana, yeye na ujumbe wake, waliwasili nchini jana kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa maazimio hayo kwa Jeshi la Polisi la Tanzania.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Inspekta Jenerali (IGP), Said Mwema, Kamishna Paul Chagonja, alisema hatua hiyo imechukuliwa na IGP Gasana baada ya kuteuliwa kushika uenyekiti wa EAPCCO katika mkutano huo.

“Baada ya kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa EAPCCO ameanza kupita nchi hadi nchi kufuatilia utekelezaji wa maazimio ya mkutano uliofanyika Kigali, mwaka jana. Tanzania ndiyo ilikuwa ya kwanza,” alisema Kamishna Chagonja. Alisema baada ya kukamilisha kazi hiyo, IGP Gasana atawaita wakuu wa majeshi ya polisi wa nchi wanachama wa EAPCCO kuwapa mrejesho.

Alisema katika mkutano wa jana kati ya maofisa waandamizi wa Jeshi la Polisi nchini na IGP Gasana na ujumbe wake, walimweleza maeneo ambayo yanahitaji msukumo hasa wa kifedha ili kuwezesha utekelezaji wa maazimio hayo, ingawa hakuyataja. 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment