Monday May 2, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

RC: Tumeshindwa kutatua mgogoro wa ardhi Zanzibar

3rd May 2012
Print
Comments

Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, wamekiri kuwa wameshindwa kumaliza mgogoro wa ardhi unaomkabili Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB), Mohamed Hashim Ismail, anayedaiwa kuvamia maeneo ya ardhi ya wananchi katika kijiji cha Pwani Mchangani, Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Pembe Khamis Juma, baada ya kutakiwa na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein, kutoa maelezo ya utekelezaji wa agizo lake la kutatua migogoro ya ardhi katika mkoa huo ili kuhakikisha haki inatendeka kwa wananchi.

Alisema Kamishna huyo wa ZRB, ameingia katika mgogoro wa ardhi dhidi ya wananchi wa eneo la Pwani Mchangani, waka 1989, wakati huo akiwa Naibu Waziri katika serikali ya awamu ya tano, ambapo alikuwa akiwatuma watu kumnunulia ardhi bila yeye mwenyewe kwenda kuona.

"Mheshimiwa Rais, ndugu Mohamed Hashim alitoa Sh. milioni 2.5 bila ya kufahamu eneo analonunua," alisema.

Hata hivyo, alisema baadaye wananchi walibaini kuwa ardhi yao imevamiwa na kuanza kuchukua hatua ya kutafuta njia ya kuikomboa lakini bila mafanikio kupitia ngazi za wilaya, mkoa na wizara husika.

Aliongeza kuwa aliyekuwa Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha, aliwahi kuingilia kati mgogoro huo, lakini alishindwa kuumaliza, baada ya Mohamed Hashim, kutoheshimu maamuzi ya Serikali ya kumtaka achukue maeneo manne ya ardhi kati ya 16 anayodai kuyanunua.

Aliongeza kuwa, juhudi zote za Serikali ziligonga mwamba, kutokana na Mohamed Hashim, kutaka kupatiwa eneo lote la ardhi aliyodai kuinunua kutoka kwa wamiliki, bila ya yeye mwenyewe kuitambua mipaka ya maeneo aliyouziwa na kusababisha Serikali kushindwa kutatua mgogoro huo.

Hata hivyo, Rais Dk. Shein alitaka kujiridhisha kwa kupata maelezo kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Mwalimu Ali Mwalimu, ambaye alisema wizara hiyo imeanzisha mpango wa kurasimisha ardhi kwa wananchi hasa wanyonge ili wawe na nyaraka halali.

Lakini alisema tatizo hilo linasababishwa na wananchi kutofahamu sheria za ardhi na wale wanaozifahamu hushindwa kuheshimu ndiyo maana wizara kuanzia sasa imeamua kupiga marufuku upimaji wa ardhi bila kushirikisha masheha, wilaya na mkoa.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles