Sunday May 26, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Makunga, Kibanda wasomewa maelezo ya awali

28th June 2012
Print
Comments
Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima, Absalom Kibanda

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es Salaam, imewasomea maelezo ya awali, Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima, Absalom Kibanda, Mhariri Mtendaji wa Mwananchi Communication Ltd (MCL), Theophil Makunga na Mwenyekiti wa Chadema Arusha, Samson Mwigamba.

Washitakiwa hao wanakabiliwa na kesi ya kudaiwa kuchochea askari polisi, magereza na wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kutotii serikali yao.

Hakimu Mkazi, Walialwande Lema, anayesikiliza kesi hiyo pia aliamuru upande wa mashtaka kuwapatia walalamikiwa wote maelezo ya mlalamikaji.

Akisoma maelezo hayo, Wakili wa Serikali, Elizabeth Kaganda, alidai  kuwa, Novemba 30, mwaka jana, washtakiwa wakitumia ujuzi na kazi yao, walichapisha kupitia gazeti la Tanzania Daima ambalo linachapishwa na kampuni ya Free Media Ltd makala iliyoandikwa na Samson Mwigamba ambaye ni mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo kuchochea askari hao kutoendelea kuitii serikali yao.

Ilidaiwa kuwa Mwigamba aliandika  waraka wenye kichwa cha habari 'Waraka maalum kwa askari wote” ambao ulisomwa na mshtakiwa Kibanda kabla ya kupelekwa kuchapishwa na kuupitisha utoke gazetini, ambapo Makunga aliuchapa bila ya kutilia maanani kwamba ulikuwa ni waraka wa kichochezi.

Kesi hiyo imepangwa kuanza kusikilizwa Agosti 7, mwaka huu.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment